Samboja AmteuaPricillah Mwangeka kama mgombea mwenza kutetea kiti chake cha Ugavana Taita Taveta

Gavana wa kaunti ya Taita Taveta Granton Samboja amemchagua , aliyekua mayor wa eneo la voi, Pricillah Mwangeka kama mgombea mwenza , kwenye azama yake ya kutetea nafasi yakuendelea kuongoza kaunti hiyo kama gavana kwa mhula wa pili.
Akiongea kwenye kikao cha hadhara eneo la mwangea mjini Voi, gavana Samboja amemtaja Pricilla kama kiongozi shupavu, ambaye kazi zake akiwa mayor wa voi zilionekana.
akiongea mda mfupi baada yake kutangazwa rasmi kama mgombea mwenza Pricillah amesema ako tayari kutekeleza majukumu watakayotwIkwa na wananchi, akielezea imani kuwa wataibuka washindi kwenye uchaguzi mkuu ujao
Ikumbukwe Hadi kuchaguliwa kwake Pricilla alikuwa akihudumu kama mshauri wa gavana Granton Samboja kwa maswala ya jinsia.