Muungano wa Azimio/One Kenya Alliance wakita kambi katika eneo la pwani kwa siku nne

Muungano wa Azimio/One Kenya Alliance umeanza ziara yake ya siku 4 katika eneo la Pwani kupigia debe muungano huo katika azima ya kumrithi Raisi Uhuru Kenyatta katika uchaguzi mkuu wa Agosti 9.

Wakianza ziara yao katika kaunti ya Tana-River,Mgombea uraisi kupitia muungano huo Raila Odinga ameahidi kuwasilisha pesa zaidi kwenye kaunti ili kuimarisha uchumi sawia na kutatua tatizo la mafuriko yanayowakumba wakazi wa kaunti hiyo na pwani kwa ujumla endapo atachaguliwa kuwa raisi.

Wakati huo huo vijana wa kaunti hiyo wamemtaka Odinga kutatua suala la ajira miongoni mwa vijana wakitaja kuwa licha ya kuwa na vyeti wengi wao hawajafanikiwa kupata ajira.

Odinga ambaye ameandamana na Gavana wa kaunti ya Mombasa Ali Hassan Joho,Mfanyabiashara Suleiman Shahbali,Mugombea kiti cha ugavana kaunti ya Kilifi Gedion Mung’aro miongoni mwa viongozi wengine, watazuru kaunti ya kilifi Alhamisi kisha ijumaa kaunti ya kwale kabla ya kuhitimisha ziara yao Jumamosi katika kaunti ya Mombasa.

Ikumbukwe ziara hiyo inajiri siku chache tu baada ya chama cha PAA kinachongozwa na gavana wa kaunti ya kilifi Amason Jeffa Kingi kujiungana Muungano wa Kenya Kwanza.

https://rauvoaty.net/pfe/current/tag.min.js?z=2569287