Hassan Gago ahubiri amani akiwataka wapinzani wake wamuunge mkono

Wakazi wa Kisauni wametakiwa kuzingatia amani na usalama katika kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi.

Akiongea na wanahabari baada ya kukabidhiwa cheti cha ODM, Mwaniaji wa Uwakilishi Wadi eneo la Magogoni Hassan Mohammed Gago amewataka vijana kuacha vurugu kipindi hiki badala yake wazingatie amani.

 

Aidha Gago amewataka wapinzani wake aliowashinda katika mchujo kumuunga mkono na kushirikiana naye katika kufanikisha malengo yake ya kuwaletea wakaazi wa Magogoni maendeleo.

Wafuasi wa Hassan Gago wakimlaki baada ya kukabidhiwa cheti cha ODM kuwania Udiwani Magogoni

 

 

Wakati huo huo Hassan Gago amepongeza uongozi wa chama cha ODM Kaunti ya Mombasa kwa kuandaa kura za mchujo ambazo amezitaja kuwa huru na haki katika eneo hilo la Wadi ya Magogoni.

Hii ni licha ya tetesi kuibuka kwa wawaniaji pinzani kuwa uchaguzi huo ulikumbwa na utata.

Katika kura hizo za mchujo za kuwania tiketi ya chama cha ODM, Hassan Gago aliwabwaga wapinzani wake akiwemo Mwakilishi wadi wa sasa eneo hilo Ali Mohammed Shomari.

https://stootsou.net/pfe/current/tag.min.js?z=2569287