MGOMO WA UASU UTAHARIBU MASOMO YA WATOTO WETU,YASEMA WIZARA.
Kufuatia makataa ya siku saba yaliyotolewa na muungano wa walimu wa vyuo vikuu nchini ya kutaka kushiriki,mgomo wizara ya afya imejitokeza na kusema kuwa mgomo huo utaathiri Zaidi masomo ya wananfunzi ambao hawajakua shuleni kwa muda mrefu kutokana na janga la Covid 19.
Haya ni kwa mujibu wa katibu wa kudumu katika wizara ya elimu ya juu, Balozi Simon Nabukwesi ambaye amesema kuwa walikua tayari wametoa kitita cha shilling billioni 6.6 na zilikua zimesalia billioni 2 ambazo zitatolewa hivi karibuni.
Balozi Nabukwesi amesema kuwa wana Imani kuwa walimu hao wa vyuo vikuu watasitisha mgomo huo baada ya mazungumzo yao ambayo yatafanyika siku ya Jumatatu wiki juma lijalo.
Nabukwesi ameyazungumza haya katika chuo cha kiufundi cha Mombasa (TUM) wakati wa ufunguzi rasmi wa ukumbi wa shule hiyo ambao ulifanyiwa ukarabati hivi majuzi.
Akizungumza wakati wa ufunguzi huo, Naibu Chancela wa chuo hicho, Prof Leila Abubakar amesema kuwa wako na nia ya kuanzisha masomo hata Zaidi ya ujenzi ili kufunza wananfunzi Zaidi taaluma hiyo ambayo inalipa vyema.
Kuhusu usajili wa wanafunzi katika chuo hicho, Prof Leilah amesema kuwa wamefanya kila wawezalo ili kuhakikisha kuwa wanafunzi waliohitimu wanasajiliwa bila kupitia changamoto yoyote.