Mbunge wa Mvita Abdulswamad amrai Rais Uhuru Kenyatta kufungua nchi kuimarisha uchumi.

Ipo haja kwa serikali kuanzisha mikakati ya ufunguzi wa taifa ikiwa ni kauli yake mbuge wa Mvita Abdulswamad sharif nassir kutokana na hali duni ya uchumi katika kaunti ya Mombasa na Pwani kwa jumla.

Katika kikao cha baraza la eid ndani ya ukumbi wa Bhadalla eneo la Spaki kaunti ya Mombasa kilichohudhuriwa na viongozi mbali mbali nchini, Abdulswamad  amemtaka kinara wa chama cha ODM Raila Odinga pamoja na Gavana wa kaunti ya Mombasa Hassan Joho kumrai rais Uhuru Kenyatta kupanga mikakati ya kufungulia sekta mbali mbali ili kuinua biashara zinazozidi kufifia ukanda wa Pwani .

Aidha Abduswamad amemtaka raisi kuhakikisha wakenya zaidi wanapata chanjo ili kurudi kuendelea na shughuli zao za kawaida huku wakizingatia masharti ya kudhibiti korona.

Kauli yake mbunge huyo iligusia aidha hali ngumu ya wafanyibiasha eneo la Mamangina na fukwe za umma ambao walifungiwa biashara zao ili kuzuia msambao zaidi wa maambukizi ya virusi vya korona nchini.

 

Hata hivyo Abduswamad amehakikishia wakenya kuwa chama cha ODM kitatoa mgombeaji wa nyadhifa ya urais na atakaye shika bendera ya chama hicho mwaka 2022 muda wowote kutoka sasa.

Abdulswamad pia amewarai wakaazi wa kaunti ya Mombasa kumchagua kuwa gavana mwaka 2022 ili kuendeleza shughuli yake ya kuwahudumia wakaazi wa Mombasa.