Seneta Faki aiomba serikali kulegeza masharti katika sekta ya usafiri wa umma kufufua uchumi

Seneta wa Mombasa Mohamed Faki amelitaka bunge la kitaifa kupitia kwa kinara wa walio wengi bungeni Amos Kimunya kuangazia kwa umakini masharti yaliyowekwa ya kupambana na corona katika magari ya umma akisema masharti hayo yameathiri uchumi na biashara hiyo kwa kiwango kikubwa.

Akizungumza katika baraza la Eidul Adh-ha lilioandaliwa katika ukumbi wa Bhadalla eneo la Spaki Kaunti ya Mombasa,Faki amesema mwezi huu wa saba kampuni tano za magari ya Ummah zimekatiza huduma zake huku maelefu ya wakenya wakipoteza kazi zao na bishara zengine kuathirika.

Faki amesema masharti ya kubeba nusu ya kiwango cha abiria tofauti na ndege na reli ya kisasa yameathiri biashara hiyo sawia na kupigwa marufuku kwa safari za usiku kwa magari ya umma.

 

Aidha seneta Faki amewarai wakaazi wa Mombasa kufanya chaguo sahihi kwa kumchagua mbunge wa sasa wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir kuwa gavana wa Mombasa ifikapo 2022 kwani utendakazi wake ni mzuri na wakupigiwa mfano na ndie mtu atakayezidi kuipeleka mbele Mombasa kimaendeleo iwapo atachaguliwa kuwa gavana.

 

Vilevile Faki amepongeza salamu za heri kati ya kinara wa chama cha ODM Raila Odinga na rais Uhuru Kenyatta akisema imesaidia pakubwa kuwaleta wakenya pamoja na kuishi kwa amani na upendo.