Wakili Khaminwa Awasilisha Ombi la Dhamana kwa Mahakama kwa ajili ya Caroline Kangogo

Chama cha mawakili nchini [LSK] kimeiomba mahamaka kuu iweze kumwachilia kwa dhamana afisa Caroline Kangogo anayeshukiwa kwa mauaji ya afisa mwenzake John Ogweno na mfanyabiashara Peter Ndwiga .

Kupitia kwa wakili John Khaminwa, LSK imerai mahakama hio kuhakikisha afisa huyo ametendewa haki ingawa bado anasalia mafichoni.

Hata hivyo, mkuu wa idara ya upelezi George Kinoti aliandaa mkutano na idara mbali mbali za uchunguzi kujadili mbinu watakazotumia kumkamata afisa huyo.

Huku haya yakijiri rais wa LSK, Nelson Havi pia amefikishwa kwenye ofisi ya Idara ya upelezi DCI kwa tuhuma  ya kumshambulia mkurugenzi mkuu wa LSK Mercy Wambua, madai ambayo Havi ameyakanusha .