Taifa Laomboleza kifo cha Seneta Yusuf Hajj hii leo

Seneta wa Garissa Mohamed Yusuf Haji ameaga dunia akiwa na umri wamiaka 80  baada ya kurejea nChini siku ya jumamosi kutoka Uturuki ambako alikuwa amelazwa tangu mwezi Disemba .

Seneta Haji  katika utumishi wa umma kwa muda mrefu tangu akihudumu kama kamishna wa Wilaya hadi alipoteuliwa katika baraza la mawaziri na baadaye kuchaguliwa kuwa seneta wa Garissa mwaka wa 2013 pia katika afisi ya mwanasheria mkuu tangu mwaka wa 1999. Haji alianza taaluma yake katika utawala  alipojiunga na utawala wa mikoa  kama D.O. mwaka wa 1960 kabla ya kuwa  mkuu wa mkoa kati ya mwaka wa 1970 na 1997

Mwaka wa 1998 aliteuliwa kuwa mbunge maalum kabla ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa Ijara  kwa tiketi ya chama cha KANU  kati ya mwaka wa 2003 na 2013, Akihudumu kama mbunge mteule  Haji aliteuliwa kuwa waziri msaidizi katika afisi ya rais  ambapo alihudumu kati ya mwaka wa 1998 hadi 2001, Baadaye alihudumu kama waziri  katika afisi ya rais anayesimamia masuala ya baraza la mawaziri mwaka wa 2002.

Baada ya ghasia za uchaguzi mwaka wa 2007/2008  Haji aliteuliwa kuwa waziri wa ulinzi chini ya utawala wa rais  mstaafu Mwai Kibaki. Mwaka  wa 2011 Haji alikuwa  nguzo muhimu katika kujadiliana kuhusu ushirikiano kati ya Kenya na Somlia kukabiliana na kundi la kigaidi la Al shabaab   na kisha baadaye kupelekea kuanzishwa kwa oparesheni Linda nchi .

Marehemu seneta huyo ni babake mkurugenzi wa mashtaka ya umma Noordin Haji  ,

Haji alizaliwa  Desemba tarehe 23 mwaka wa 1940, alitoka ukoo  mdogo wa Abdalla wa uKoo mkubwa wa Ogaden  na mamake alikuwa Mborana .

Seneta huyo ataswaliwa Masjid Noor SOUTH C Nairobi na kuzikwa katika maziara ya Langata saa kumi jioni

Mwandishi: Charles Omondi