Gharama ya umeme Yazua Changamoto,Uhaba wa maji Kilifi

Serikali ya kaunti ya Kilifi kwa ushirikiano na wadau wa sekta ya maji na usafi nchini imeanzisha zoezi la kuboresha huduma za maji na usafi katika mji wa Malindi na kaunti ya Kilifi kwa jumla.

Sekta hii imekumbwa na changamoto ya uhaba wa maji wa mara kwa mara sasa huku wakaazi wakilalamikia uzembe, ufisadi na deni la stima katika kampuni ya maji na maji taka hata baada ya kampuni hiyo kulipa zaidi ya shilingi milioni 40 kila mwezi.

Kwa upande wake mkurugenzi mkuu katika kampuni ya maji Gerald Mwambire amekiri kuwa tatizo la umeme ni changamoto kubwa kutokana na bili ya stima kupanda.

Hali kadhalika,naibu wa gavana Gideon Saburi amesema kuwa bili zinapoongezeka ,hawapati nafasi ya kujadiliana kama washikadau “Bill zinapoaccumulate mara moja hautupi nafasi nzuri ya kujadiliana kama washikadau.” hata hivyo, shilingi bilioni mbili zimetengwa na serikali ya kaunti ili kuimarisha sekta hii.

Milioni mia saba aidha, zimetengwa ili kuboresha miundo msingi ya mabomba ya maji hasa ndani ya miji.

wadau katika sekta ya usafi nchini wamefurahia kuzinduliwa kwa mpango huo na wameahidi ushirikiano katika Nyanja hiyo.

Mwandishi: Mariam Swaleh