Pendekezo la kuongezwa kwa karo kwenye vyuo vikuu yazua hisia mseto

Wanafunzi wa chuo kikuu cha Nairobi wakiandamana Picha kwa Hisani

Vyuo vikuu vingi vya umma vimekuwa vikijitahidi kufikia gharama zao za kutoa huduma kila siku kwa sababu ya kuporomoka kwa mapato na upungufu wa ufadhili wa serikali.

Taifa kwa sasa inakabiliwa na maswala tofauti kama ugonjwa wa
Corona, ufisadi, na ukosefu wa ajira ambayo inasababisha idadi kubwa ya watu wanaoishi na umaskinikuathirika kiuchumi hali inayotokana na kupungua kwa ufadhili wa serikali.

Wanafunzi wa vyuo vikuu wamekuwa wakilipa ada sawa shuleni kwa
miaka mingi, hata hivyo nyakati nazo zimebadilika, huku gharama ya
maisha na kufanya biashara imepanda.

Vilevile, imekuwa ngumu kwa vyuo vikuu vya umma kuendelea na
shughuli zao huku wengi wanahangaika kulipa mishahara ya
wafanyikazi ambayo imekuwa nadra kwao kupambana na hali hii.

Kwa bahati mbaya, wahadhiri wanaotoa mafunzo huenda kwa muda
mrefu bila malipo,halkadhalika taasisi zingine zinadaiwa maelfu ya
shilingi katika malimbikizo ya malipo ambayo wameshindwa kulipa.

Aidha, hali hii huwavunja morali na kuathiri ubora wa utendaji kazi.
Kwani ni ngumu kwa wahadhiri kufanya utafiti unaozalisha pesa kwa
sababu ya mzigo mzito wa kazi, haswa katika taasisi zinazosimamia
utafiti.

Haishangazi kupata kwamba wanafunzi wengi kutoka familia
zisizojiweza, hawawezi kumudu gharama za kuishi chuoni, hata kwa ada kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HELB) kwani wengi wa
wanafunzi hutegemea sana fedha kutoka kwa bodi hiyo.

Licha ya kuongezeka kwa ada ya masomo kuna haja ya kushirikisha
washikadau wote kufikia makubaliano juu ya njia ya kuhakikisha
uendelevu wa vyuo vikuu na kuhakikisha mifuko ya wazazi haitaumia.

Mwandishi: Ken Wanje