Hospitali ya Aga Khan yapiga marufuku barakoa zinazochuja hewa

Hospitali ya Chuo Kikuu cha Aga Khan imeunga mkona Shirika
la Afya Ulimwenguni (WHO) na kupiga marufuku utumiaji wa
maski zenye vishimo vya kumulia ndani ya majengo yake.

Kulingana na utafiti uliofanywa na hospitali hiyo na kuanda
hotuba hapo jumatano, ubunifu wa barakoa hizo huruhusu
uchujaji wa hewa ya kuvuta pumzi na kuacha hewa inayotolewa
nje.

Hospitali hiyo imedai kuwa hewa inayotolewa inaweza
kusambaza viini vinavyosababisha virusi vya Corona kutoka
kwa mtu asiyevaa barakoa, kwani zinauwezo wa kulinda
wanaozivaa wala si waliokaribu nao.

Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) halishauri kabisa utumiaji
wa maski zenye vishimo vya kupumulia. Kulingana na nao,
maski hizo zinakusudiwa wafanyikazi wa viwandani kuzuia
vumbi na chembechembe kupulizwa hewani.

Hii inafanya barakoa kutokuwa na ufanisi unaofaa katika kuzuia
kuenea kwa ugonjwa wa COVID-19 au virusi vyovyote vya
kupumua, taarifa hii ilitolewa kwenye wavuti ya Shirika la Afya
Ulimwenguni (WHO).

COVID-19 huenea haswa kupitia matone ya kupumua wakati
wa mazungumzo, pale mtu anapopiga chafya au kukohoa, na
haya yote yanaweza kuzuiliwa na uvaaji wa barakoa saa zote.

Mwandishi: Ken Wanje