Mashirika Yatuzwa Nchini Ulimwengu Ukiadhimisha Siku ya Haki za Kibinadamu.

Hii leo Kenya imejumuika na ulimwengu kuadhimisha siku ya Haki za Kibinadamu (Human Rights). Huku kauli mbiu ikiwa simama kutetea haki za kibinadamu.

Shirika la Haki Yetu limechukua mkondo wa kuwazawadi wakereketwa mbalimbali kwa hatua walizopiga kutetea haki za kibinadamu na kuhakikisha sheria zinalindwa.

Katika sherehe hiyo wameweza kuwatuza watu na mashirika katika vitengo mbali mbali  ikiwemo Child Protection iliyokabidhiwa  Patroba Ondiek, Helda Esily akizawadiwa  Katika kitengo cha kukabili  dhulma za kijinsia, Uongozi wa Vijana akipewa Esther Muthoni , Tuzo la amani na elimu ya kijamii zikiwaangukia Francis Katana na Dennis Kazungu Mtawalia.

Aidha tuzo la shirika la  kutetea maeneo ya uvuvi pamoja  na shirika kutetea haki za ardhi kubabidhiwa Mercy Mghanga na Joyce Mwasaru huku tuzo maalum likimuangukia mwenyekiti wa muungano wa mashirika ya kijamii Zedekia Adika.

Akizungumza na Radio Salaam Mkuu wa mipango wa Haki Yetu Peter kazungu, amesema kuwa Taifa imelegeza kamba katika masuala ya kutetea haki za kibinadamu katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya afya na usalama.

Hata hivyo Adika amewahamasisha wanajamii kuweza kushikana mikono ili waweze kupeleka nchi ya Kenya Mbele.

https://moonoafy.net/pfe/current/tag.min.js?z=2569287