Mashirika yavaa Magwanda Kuinua Watoto Kupitia Kinamama, Mombasa

Shirika la Kimataifa la kutetea Haki za watoto la ARIGATOU kwa ushirikiano na shirika la kutetea jamii Duniani GCERF limeanzisha mchakato wa kuwainua watoto kupitia kwa wamama kaunti ya Mombasa .

Mshirikishi wa shirika hilo hapa Kenya Dkt. Dorcas Kiplagat amesema watoto wengi wanapitia dhulma kutokana upungufu wa maswala kadhaa ikiwemo janga la corona ambayo imeshuhudia watoto wengi kunajisiwa na wengine kuwa waja wazito.

Aidha Dorcas ametaja hatua ya kuelimisha familia kupitia akinamama ni njia bora kupata suluhu ambapo takriban wamama mia 8 kaunti ya Mombasa wamepewa mafunzo jinsi ya kupamba ghasia za familia pamoja na hatua wanazopaswa kuchukuwa.

Vile vile wanawake 100 wamesajiliwa kama viongozi kueneza agenda za shirika hilo hususan eneo la Kisauni na kuendeleza biashara ndogo ndogo kuinua familia za watoto hao.

Mwandishi: Charles Omondi