Steji ya Matatu Liwatoni Yapingwa Wakaazi Wakitishia Kuandamana

wakaazi wa Liwatoni- Ganjoni Kaunti ndogo ya Mvita wameitaka serekali kusitisha ujenzi wa kituo cha kuabiri magari bila kuwashirikisha.
wameitaka serekali kufutilia mbali mradi huo na kutishia kwenda kotini iwapo serekali haitaingilia kati kwani wanakadiria hasara kubwa ambayo wanakisia itaathiri maeneo hayo na usalama wa wakaazi kwa jumla .
wakaazi waliwatoni wanakadiria maandamano mengine ya Amani juma lijalo licha ya haya kutokufanyika kwa kukosa kuwasilisha barua ya maandamano mapema .
Seneti wa Mombasa Mohammed Faki amesema kuwa hawajaona manufaa ya mradi huo licha ya kuwa hawakupewa taarifa dhidi ya ujenzi wa kituo hicho
Mwandishi: Mwanaisha Dzame