Wafanyakazi wa afya,Nandi wahamasishwa kuhusu afya

Serekali ya kaunti ya Nandi  pamoja na shirika la haki na usawa (Equality Now) wameanda kikao cha siku mbili kwa wafanyakazi wa afya katika jamii ili kuwafunza namna ya kukabiliana na  dhulma za kijinsia na mimba za mapema.

Hii ni baada ya ongezeko la visa vya mimba za mapema na dhulma za kijinsia kuripotiwa miongoni mwa  wakaazi wa kaunti ya Nandi .

Makundi mbali mbali yalishawishiwa kujitolea na kuhakikisha sauti  na maoni kuhusu dhulma za  kijinsia yanatiliwa mkazo katika  kaunti hiyo.

Vile vile,serekali ya kaunti ya  Nandi inapania kubuni sera mbadala ya kulinda watoto na wakaazi kwa jumla kutokana na dhulma hizo .