Sossion aitaka serikali kutoa fedha kwa shule

Katibu wa KNUT Wilson Sossion Picha kwa hisani

Katibu mkuu wa chama cha walimu nchini (KNUT) Wilson Sossion ameitaka serikali kutoa fedha kwa shule ili kuzisaidia kupambana na makali ya korona .

Sossion amesema shule hazikupatiwa hata shilingi zilipofunguliwa hivyo kuchangia ongezeko la maambukizi ya korona shuleni.

“kama serikali haiwezi toa vifaa vya kujilinda kwa wanafunzi na walimu basi hamna kitu wanachofanya,” amesema Sossion.

Amesikitishwa na hali ya baadhi ya wanafunzi kukosa barakoa na vifaa vingine vya kujilinda dhidi ya maambukizi hivyo basi kuwa vigumu kwa walimu kuwafunza namna ya kujikinga.

Serikali imeombwa itoe shilingi bilioni tatu kwa shule endapo inathamini maisha ya walimu na wanafunzi.

Mgogoro wa tume ya kuwaajiri walimu nchini na chama cha KNUT ulijitokeza wazi wazi , katibu huyo akisikitishwa na hatua ya mwajiri wao TSC kutoheshibu mkataba kati yao.

Tangu Julai 1,2019 tume ya kuwaajiri walimu (TSC) imefungia nje walimu wanachama wa KNUT uwezo wa kuongezwa mshahara na kupandishwa vyeo.

Hatua hiyo imenyima walimu haki ya kuwa kwenye miungano ,zaidi ya walimu 180,000 wakijitoa kwa KNUT.

KNUT imemwandikia waziri wa leba ikimtaka kutatua shida hiyo ndani ya siku saba la sivyo waichukulie hatua TSC.