zaidi ya watu 500 wadhibitishwa kuwa na korona

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe Picha kwa hisani kutoka Twitter

Watu 559 wapya wamedhibitiwa kuambukizwa virusi vya corona na kuongeza idadi kuwa 70,808

541 ni wakenya , 18 wakiwa watu wa mataifa ya kigeni. 336 wakiwa wanaume ilhali 223 wakiwa wanawake.
Akihutubia vyombo vya habari, waziri wa afya Mutahi Kagwe amesema watu 478 wamepona.

Miongoni mwao pamekuwa na watu 337 wamekuwa wakipokea matibabu nyumbani huku wenzao 141 waliokuwa hospitalini wakiruhusiwa kwenda nyumbani.

Wagonjwa 18 wamepoteza maisha yao chini ya saa 24 na kuongeza idadi hiyo kuwa 1,287.

Malalamishi ya wahudumu wa afya yamezungumziwa, waziri Kagwe akiamuru bima ya afya ya taifa NHIF kukamilisha mazungumzo kuhusu bima kwa madaktari na kutoa mwelekeo kesho Jumanne ya Novemba 17, 2020.

Kamati ya dharura kuhusu msambao wa korona kwenye kaunti zimeagizwa kufanya mikutano na kuja na mikakati itakayozuia msambao wa korona kwenye kaunti hizo na kushirikiana na asasi za usalama kuhakikisha utekelezwaji wa sheria hizo.

Ametaka kamati hizo , kupiga msasa uwepo wa mitungi ya hewa safi na vifaa vya madaktari vya kujilinda dhidi ya maambukizi na kuripoti upungufu wowote wa vifaa hivyo.

Waziri huyo amesikitishwa na hatua ya wakenya kupuuza masharti ya kuzuia msambao wa korona wanapokongamana hususan harusini na matangani.