Kenya kwenye nafasi ya 113 katika ustawi wa uchumi ulimwengu

Picha kwa hisani

Kenya imeshuka kwa ustawishaji uchumi kwa alama 1 na kuangukia nafasi ya 113 kati ya mataifa 167 ulimwenguni.

Hii ni kulingana na shirika la kujadili takwimu iliyofanywa na taasisi ya Legatum ambayo imebaini Kenya kuongeza umaarufu kwa pointi 51 kutoka pointi 46 mwaka wa 2010 Nchi imesajili faida kubwa katika upigaji kura wake juu ya uaminifu wa taasisi , utulivu wa uchumi kwa jumla, hatua za kiafya, uhusiano, haki za mali na ulinzi wa wawekezaji .

Mataifa kadhaa ughaibuni zimeratibiwa kuchukuwa nafasi 10 za kwanza kiuchumi huku Syria, Sudan, Eritrea, DRC, Afghanistan, Somalia, Chad, Yemen na Congo ya kati ikichukuwa nafasi tisa za chini kulingana na taasisi hiyo.

Mafanikio ya ustawi hata hivyo sasa yanatishiwa na janga la corona ambalo linatishia kufuta mafanikio yaliyopatikana katika muongo mmoja uliopita .