Wanafunzi kurudi shuleni mapema mwakani

waziri wa elimu Profesa George Magoha pamoja na washikadau akihutubia wanahabari Picha kwa hisani ya twitter, wizara ya Elimu

Sasa ni rasmi kuwa wanafunzi wote wakiwemo wale wa shule za kimataifa watarudi shuleni tahere 4 mwezi January mwaka ujao 2021 , wanafunzi wa gredi ya kwanza, ya pili na ya tatu na wale wa darasa la 5, la 6 na la 7 pamoja na wa kidato cha kwanza, cha pili na cha tatu wakitarajiwa kuanza muhula wa pili.

Waziri wa elimu Profesa George Magoha ametoa ratiba na muongozo kuhusu ufunguzi wa shule za msingi na sekondari Kama alivyoagiza rais Uhuru Kenyatta wiki jana alipokuwa akihutubia taifa.

Wanafunzi wote isipokuwa wale wa darasa na nane na kidato cha 4 watakuwa na likizo ya wiki saba kupisha mitihani ya kitaifa ya KCPE na KCSE.

Wale wa chekechea watakaotimu miaka minne wataripoti Julai, 2021 huku Gredi ya nne wataingia gredi ya tano Julai, 2021 wakichukua likizo fupi na wenzao wa kidato cha kwanza wapya huku wenzao wakiendelea na muhula wa tatu.

Magoha ametoa hakikisho kuwa serikali italinda afya ya walimu na wanafunzi watakapokuwa shuleni, aidha amewashukuru wazazi, serikali za kaunti na washikadau kwa kuhakikisha kuwa shule zimezingatia kanuni za wizara ya afya za kudhibiti msambao wa Covid-19.