Bidha ghusi zenye thamani ya milioni mia moja zachomwa

Mwenyekiti wa mamlaka ya  kudhibiti bidha ghushi nchini Florah Mutahi ameongoza zoezi la kuchoma bidha ghushi zenye thamani ya shilingi milioni mia moja huko Saimbot, Port Rietz.

Bidha zilizochomwa kulingana na kanuni za wizara ya mazingira zilijumuisha vifaa vya kudhibibiti msambao wa virusi vya korona, simu, vifaa vya kielektroniki,vifaa vya kujenga , kemikali miongoni mwa bidha zingine.

Florah aidha amesema kuwa asilimia sabini ya bidha hizo ni za kutoka mataifa ya nje na kuongeza kuwa wamechoma bidha zenye thamani ya takribani bilioni moja nukta nne kwa miaka tano.

Vile vile  Alitilia shaka uwepo wa bidha ghushi sokoni unaofifisha sekta ya uzalishaji. Kazi 1,700 zimepotezwa kwenye sekta ya uzalishaji kufwatia uwepo wa bidhaa hizo.

Kwa upande wake Kamishna wa mkoa wa Pwani  John Elunguta ambaye alikuwa kwenye zoezi hilo amesema kuwa serikali imewekeza fedha za kukabiliana na changamoto hiyo na kuwa watakaopatikana watatajwa hadharani.

Elungata Ameongezea kuwa polisi wako chonjo na pamoja na maafisa wa jinai , kitengo cha ujasusi , walinzi wa bahari pamoja  bandari na walinzi wa ferry hawatoruhusu bidha hizo kuingia nchini.

Kaunti ya  Mombasa imetajwa kama eneo linaloathirika pakubwa na uwepo wa bidha hizo kwa sababu ya uwepo wa bandari inaoingiza bidha kutoka nje.

Hata hivyo Elungata Amehimiza wananchi kuchunguza bidha kabla ya kununua na wafwate vigezo vya halmashauri ya kuhifadhi mazingira(NEMA) na mamlaka ya ujenzi nchini (NCA) wanaponunua bidha za ujenzi na wakitilia shaka bidha hizo wawaarifu polisi.

 

 

 

https://moonoafy.net/pfe/current/tag.min.js?z=2569287