Viongozi kutoka jamii za wafugaji waunga mkono BBI

Kiongozi wa ODM Raila Odinga akiwahutubia viongozi kutoka jamii za wafugaji Picha kutoka Twitter

Viongozi kutoka jamii za wafugaji wameapa kuunga mkono ripoti ya jopo la BBI.

Wakiongozwa na waziri wa Fedha Ukur Yatani , na mbunge wa Eldas Aden Keynan, viongozi hao walisema kuwa waliafikia uamuzi huo baada ya kufanya mikutano na kiongozi wa ODM Raila Odinga aliyekubali kusikia na kujumuisha matakwa yao kwenye ripoti hiyo.

Awali viongozi hao walilalama kuwa maswala yao hayakuzingatiwa kwenye ripoti hiyo ikiwemo maswala ya mifugo , ugavi wa fedha na rasilimali.

Kwa upande wake, Raila Odinga ambaye ni muasisi wa ripoti hiyo amekubali kuteuliwa kwa viongozi watatu watakaoshauriana na jopo la BBI na kuhakikisha kuwa maswala yao yamejumuishwa kikamilifu kwenye mchakato wa BBI.

Raila vilevile amepigia debe ripoti ya BBI akisema kuwa itatatua shida na changamoto zinazozikumbuka nchi hii.