Mashirika ya kutetea haki za binadamu yaitaka serikali kudumisha haki ya kuandamana

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yamekongamana mjini Mombasa kukashifu hatua ya serikali na vyombo vya usalama kutoheshimu na kutozingatia haki ya binadamu ya kuandamana haswa katika kaunti ya Mombasa.

Wakiongozwa na Suba Churchill kutoka shirika la Civil Society Reference group (CSRG) wamesisitiza kuwa kuandamana ni haki yao k na kuwa asasi za usalama zinawatawanya na kuwapiga wanapoandama licha ya kuwa wamefwata sharia na kuzingatia masharti ya kukabidhi covid-19.

Walitaja maandamano yaliyofanyika tarehe 25 Agosti mwaka huu kama mojawapo ya visa ambapo polisi hawakudumisha haki zao.

Maandamano hayo yalinuia kukemea uwizi wa fedha za umma katika shirika la KEMSA iliyoishia kwa watu sita walikamatwa.

Mashirika hayo yanayojumuisha Article 19 Africa mashariki,CSRG,MUHURI, Kituo cha Sheria na Social Justice Centre , Mombasa, yamefanya mikutano na vyombo vya usalama na kutoa malalamishi yao.

Kwenye mikutano hiyo waliitaka asasi za usalama kutotumia Covid-19 kama sababu ya kuwazuia wakaazi wa Mombasa na Kenya kwa jumla kutoandamana na kukashifu vitendo vya ufisadi nchini.

Wametishia kupeleka kortini polisi wanaotumia nguvu kupitia kiasi endapo hawatazingatia na kudumisha haki za binadamu kwenye maandamano.