Rais Uhuru Kenyatta apokeza wakaazi wa Samburu hati miliki za ardhi

Rais Uhuru Kenyatta na Waziri wa ardhi Faridah Koroney picha kwa hisani ya PSCU

Rais Uhuru Kenyatta ameongoza hafla ya kupokeza wananchi wa eneo la Samburu hatimiliki za ardhi bila malipo.

Rais amesema kuwa hatua hiyo itachangia pakubwa kuboresha maisha ya wakenya.

Amesema kuwa mwananchi akiwezeshwa kumiliki ardhi yake , anaweza kuigeuza na kuwa yenye manufaa kwake.

Ameongezea kuwa hatua hiyo italeta mabadiliko kwa kuwa hawatakuwa na hofu ya kufurushwa kutoka kwa ardhi yao .

Swala la ardhi la jamii liligusiwa na rais huku akitaka wananchi wapewe hatimiliki za ardhi hizo na viongozi wao waamue namna ardhi hizo zitakavyotumika kulingana na matakwa ya wananchi.

Viongozi na wananchi wamehimizwa na rais kutafuta wawekezaji watakaowekeza kwenye ardhi hizo na kupuni nafasi za kazi kwa vijana na wananchi.

Wananchi wa eneo la Samburu walimpongeza rais kwa hatua hiyo na kusifia utendakazi wake.

Wakenya zaidi ya milioni tano wamefaidika na hatua hiyo ya serikali kutoa hati miliki za ardhi bila malipo.