Gavana Mutua asisitiza kuwa ‘handshake’ haitotoa umaskini nchini

Gavana Alffred Mutua akiwa kwanye mojawapo ya kampeni zake picha /kwa hisani

Gavana wa kaunti ya Machakos Alfred Mutua amesisitiza kuwa mswada Utangamano BBi utafeli endapo haitahusisha wakenya wote kikamilifu

Gavana Alfred Mutua ni kiongozi wa hivi punde kutoa hisia zake kwa ripoti hio ya jopo la upatanishi BBI.

Akizungumza mjini Mombasa na wanahabari , Mutua amesema kuwa ripoti hiyo itafeli endapo haitahusisha wote. Ametaja kuwa viongozi wote wanapaswa kuhusishwa ili wajue ni vipengele vipii vya BBI vinafaa kwa wananchi.

Gavana Mutua anasema kuwa ‘Handshake’ si njia mwafaka ya kutoa umaskini nchini akiongezea kuwa serikali haijakuwa ikiwajali wananchi wake kwa muda.

Mutua aidha, alitilia shaka viwango vya umaskini nchini , akitaja uwepo wa upungufu wa kazi na mzunguko duni wa fedha nchini huku akitoa wito kwa wanyonge na vijana kuweza kupata kazi.

Kiongozi huyo vilevile amesema kuwa ripoti hiyo inahatma wastani itafaulu au kuanguka kulingana na maamuzi ya wakenya.

Kauli ya kiongozi inajitokeza siku chache baada ya rais Uhuru Kenyataa na Kinara wa ODM Raila Odinga kupokea ripoti hiyo katika ikulu ndogo ya Kisii na kutarajiwa kuzinduliwa rasmi tarehe 26 Oktoba katika ukumbi wa Bomas of Kenya, Nairobi.

Hata hivyo msafara wa kiongozi huyu unatarajiwa kuzuru maeneo ya Majengo, Kongowea,Mtwapa na Kilifi wikii ijayo.

Mwandishi: John Otieno