Rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga Wapokezwa ripoti ya BBI Kisii

Mchakato wa BBI umerudi tena Rasmi baada ya ripoti hiyo kupokezwa kwa Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga hii leo kutoka kwa kamati iliongozwa na seneta wa Garisa Yusuf Haji.

Ripoti hiyo iliyokuwa gumzo miongozi mwa wanasiasa imekuwa ikisubiriwa kwa hamu na ghamu na wakenya mbali mbali kote nchini.

Katika mkutano uliofanyika ikulu ndogo katika kaunti ya kisii Rais Kenyatta alisema kuwa ripoti hiyo ni ya wakenya wote na si ya mtu binafsi huku akiwasihi wakenya kuisoma na kutoa mchango wao wakiwa na nia ya kuiboresha bila ya  kuzua mtafaruko.

Uhuru  aidha, alifutilia mbali madai ya kwamba anajitafutia nafasi ya kisiasa kupitia mchakato huo na kuongeza kuwa huu si wakati wa kuleta tofauti baina ya wakenya

Vile vile Raila Odinga alifutilia mbali kauli potofu kuhusu mswada huo wa BBI na kukiri kuwa ripoti hiyo inanuia kuleta utangamano nchini na ndiyo njia ya kuikomboa kenya.

Hata hivyo Ripoti  hiyo ilipendekeza mambo kadha ikiwemo;

  • Kuwepo kwa ofisi ya waziri mkuu na mawaibu wake wawili na Mawaziri kuteuliwa miongoni mwa wabunge.
  • Kubuniwa kwa tume ya huduma za Afya .
  • Kubuniwa kwa msajili wa malalamishi katika idara ya mahakama atakayepokea malalamishi kutoka kwa wakenya kuhusu idara ya mahakama na kuyachunguza.
  • Wanafunzi wa chuo kikuu kupewa muda wa miaka minne baada ya maliza chuo kikuu kabla ya kuangazia kulipia mkopo huo miongoni.

Kwa sasa mpira upo mikononi mwa wabunge iwapo wataupitisha mswada huo wa BBI  utakapofikishwa bungeni na kuwapelekewa wakenya debeni kwenye kura ya maamuzi , kuipitisha ama kuiangusha ripoti hiyo.

Mwandishi : John Otieno