HAKI AFRICA yaiandikia IEBC ikiitaka ihairishe uchaguzi wa msambweni

Barua ya Haki Africa kwa mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati

Kupitia kwa mkurugenzi wao ,shirika la Haki Africa limemwandikia barua Wafula Chebukati Mwenyekiti wa tume ya Uchaguzi nchini (IEBC) ikimtaka kuhairisha uchaguzi wa eneo bunge la Msambweni inayotarajiwa kufanyika tarehe 15 Disemba mwaka huu.

Shirika hilo linasema kuwa wanasiasa wameweka maisha ya watu wa Msambweni hatarini ya kuambukizwa virusi vya Korona kupitia mikutano ya siasa isiyozingatia sheria na mikakati iliyowekwa na wizara ya afya nchini kudhibiti msambao wa virus ihivyo.

“Haki Africa inatoa wito uchaguzi wa eneo bunge la Msambweni kuhairishwa. Hii ni kwa sababu ya wingu la pili la msambao wa virusi vya korona ambao umechangiwa na siasa mbaya Msambweni,mkoa wa Pwani na nchini kwa ujumla,” sehemu ya barua hiyo inanuku.

Akiongea na wanahabari kwenye afisi za shirika hilo, mkurugenzi wa shirika hilo Hussein Khalid anawatupia lawama Polisi kwa utepetevu wao na kutochukulia hatua wanasiasa wanaovunja sheria zilizowekwa kudhibiti msambao wa korona.Alitoa wito kwa polisi kuwa tia mbaroni wanasiasa watakaopatikana wakivunja sheria hizo.

“Tunatoa wito kwa polisi kuwakamata viongozi wanaohusika kwenye oparesheni hiyo (kuanda mikutano ya siasa) wakiongozwa na Raila Odinga na William Ruto ambao wanajihusisha pakubwa kwenye kampeni hizo,”alisema bwana Hussein.

Hussein anataka uchaguzi huo usitishwe kwa muda hadi pale ambapo visa vya msambao wa korona vitapungua.
Amesisitiza kuwa afya ya wananchi sharti ipewe kipaumbele.

John 0tieno