"> Musikubali kutumiwa kisiasa, Asema Machele. – Salaam Fm

Musikubali kutumiwa kisiasa, Asema Machele.

Huku mwaka wa uchaguzi ukikaribia wanaomezea mate viti mbali mbali wamehimizwa kupelekea wananchi wao miradi ya maendeleo na wala sio kueneza siasa za chuki.

Haya ni kwa mujibu wa Patron wa Wakfu wa Machele, Mohammed Soud Machele ambaye amesisitiza kuwa ni lazima wananchi wafaidike na miradi ya maendeleo na wala sio siasa zisiozo kuwa na msingi.

Machele ameongezea kuwa baadhi ya vijana wamekua wakitumiwa na wanasiasa kwa kupewa pesa kutukana viongozi wengine katika mitandao ya kijamii jambo ambalo anasema kuwa halifai hata kidogo.

 

Machele aliyazungumza haya wikendi hii wakati wa kupeana tanki za maji kwa kikundi cha Al -Wahda kutoka eneo la Kaloleni katika eneo bunge la Mvita.