"> Mtoto wa Kike Athirika Pakubwa na Duluma za Kijinsia, Yabaini Mashirika ya Kijamii, Mombasa – Salaam Fm

Mtoto wa Kike Athirika Pakubwa na Duluma za Kijinsia, Yabaini Mashirika ya Kijamii, Mombasa

Shirika la vijana la Stretchers limeungana pamoja na mashirika mengine ili kuweza kujadili changamoto anazopitia mtoto wa kike hususan katika kipindi hiki cha Corona.

Wakiongozwa na mmoja wa wafanyakazi wa shirika hilo Dickson Okongo ameeleza kuwa  Stretchers imebaini kuwa watoto wa kike ni miongoni mwa  walioathirika pakubwa kutokana na dhulma za kijinsia hivyo basi ipo haja ya mashirika mbalimbali kuja pamoja ili kuweza kupata suluhu.

Kwa upande wake mwenyekiti wa shirika linalojihusisha na uhifadhi wa sodo kwa njia bora Catherine Wanjoya amesema kuwa   masuala ya hedhi hayajangaziwa kwa kina kutokana na tamaduni pamoja na mila tofauti kwa baadhi ya jamii.Aidha Wanjoya ameitaka jamii kumhusisha mtoto wa kike katika kufanya maamuzi.

Hata hivyo  wito umetolewa   kwa jamii  kushirikiana ili kuweza kuwasaidia watoto wa kike wanapokuwa katika siku zao za mwezi vilevile wameongeza kuwa jamii  inapaswa kutupilia mbalii tamaduni potovu.