"> Serikali Yatakiwa kutoa Mwelekeo Kufungua Taasis za Kidini – Salaam Fm

Serikali Yatakiwa kutoa Mwelekeo Kufungua Taasis za Kidini

Shirika la kenya muslim youth alliance inapendekeza serikali kutoa mwelekeo mwafaka kwa ufunguzi wa taasisi za kidini za elimu nchini.

Wakiongozwa na Khamisi Akbar Mwaguzo, shirika hilo limesikitishwa na hatua ya serikali kuweka mikakati ya ufunguzi wa shule na kusahau taasisi za kidini ikiwemo Sunday schools na Madrasa baada ya kufungwa mwanzoni mwa mwaka kuzuia maambukizi ya korona .

Aidha Mwaguzo amesisitiza kuwa lazima walumu wa taasisi hizi wapehaki zao kama wengine na kuwaruhusu kuwatayaisha watoto kwa ajili ya masomo ya kidini kwa kuzingatia kanuni zilizowekwa na wizara ya afya.