Baraza la usalama Laapa Kuchukulia Hatua kwa Wachochezi
Baraza la usalama nchini limetoa onyo kwa wanasiasa wanaotumia vijana kujinufaisha kisiasa.
Mwenyekiti wa baraza hilo ambaye pia ni mkuu wa huduma kwa umma Joseph Kinyua ametaja wanasiasa kuwa chanzo cha vurugu humu nchini huku wakitaja vikwazo watakaochukuwa kuwakabili wanasiasa hao ikiwemo kuchukuwa kibali kutoka kwa afisa wa kituo cha polisi OCS.
Aidha baraza hilo limetaka watakaohudhuria hafla ya kisiasa kukabidhiwa polisi watakaochunguza ndimi za chuki huku vyombo vya habari vikionywa kueneza habari za kugonganisha watu.
Hatua hii inazuka baada ya ghasia za kisiasa zilizoshuhudiwa huko Muranga ambapo watu 2 walifariki katika hafla ya ibada iliyohudhuriwa na naibu Rais William Ruto.