"> ‘Ahueni ya Ushuru Usalie Chini’ Yasema ICPAK – Salaam Fm

‘Ahueni ya Ushuru Usalie Chini’ Yasema ICPAK

Taasisi ya kuidhinisha mahasibu nchini ICPAK  imeitaka bunge la taifa pamoja na Rais Uhuru Kenyatta kuzidisha afueni ya ushuru kwa muda wa miaka 2 .

Akizungumza kwenye mkutano uliofanyika katika hoteli Sarova White Sands  na mahasibu kutoka kaunti mbali mbali nchini, Mwenyekiti wa Taasisi hiyo  Rose Mwaura anapendekeza Kamishna Mkuu kuangazia tena  ilani iliyochapishwa kwenye gazeti la kitaifa  na marekebisho ya mfumko ili kudumisha viwango vya sasa kwa ushuru  na kukagua kundi la bidhaa zilizo na mguso kubwa kwa umma kama maji ya chupa na mafuta.

Aidha serikali imetakiwa kuondoa vipimo vya kupitiliza ilikukabili utumizi mbaya na ufujaji wa raslimali ya umma ikiwa ni pamoja na kuwa na uwazi katika mchakato wa ununuzi wa umma kama ilivyopendekezwa na  Rais baada ya kashfa ya KEMSA.

Hata hivyo Kitengo cha upelelezi nchini pamoja na Afisi ya mkurugenzi wa mashtaka y umma ODPP wametakiwa kuangazia kwa haraka utumizi mbaya wa hazina na kupeleleza walishtakiwa kufuja hazina hii na hatua kali kuchukuliwa kwa wahusika wake.