"> Habari mseto za Uchumi na Biashara. – Salaam Fm

Habari mseto za Uchumi na Biashara.

Tutafikia malengo yetu ya kusanya Ushuru licha ya changamoto: KRA

Mamlaka ya kukusanya ushuru nchini KRA inataraji kwamba shughuli ya kukusanya ushuru nchini itaimarika tena, baada ya viwango vya maambukizi  vya virusi vya Corona kuanza kupungua pamoja na kulegezwa kwa baadhi ya masharti ya kuthibiti korona.

Naibu kamishna wa KRA anayehusika Na ushuru wa ndani Caxtone Masudi, anasema  tayari KRA imeona mabadiliko makubwa, katika viwango vya ushuru vinavyokusanywa kati ya Julai na Septemba.

kwa sasa viwango vya ushuru tunayo kusanya imeanza kuongezeka, tunaamini kuwa tutafikia malengo yetu mwishoni mwa mwaka wa kifedha” alisema Bw. Masudi

Kadhalika Masudi amesema KRA ingali imelenga kukusanya shilingi trilioni 1.52 katika ushuru wa kawaida  kwa mwaka wa kifedha wa 2020/2021 ambayo itakamilika Juni mwaka ujao.Hatua ya juzi ya serikali ya kuruhusu kufunguliwa kwa biashara za baa na vilabu vya burudani, inatarajiwa kuongeza viwango vya ushuru vinavyokusanywa nchini.

 

Hatua za kuinua Tuskeys za pamba moto, macho yote kwa Okumu.

Tuskys Supermarket along Kenyatta Avenue in Nairobi on July 18,2019 where the meat section was closed on Suspicion that the meat had excess chemical additives.EVANS HABIL

Kampuni ya Jumla inayokabiliwa na utata nchini Tuskeys, imemteua aliyekuwa  afisa mkuu wa masuala ya kifedha kwenye maduka ya Uchumi Fredrick Omondi Okumu, kuwa afisa wake wa masuala ya kifedha wakati ambapo Tuskeys inafanya juhudi kujiinua.

Okumu ambaye ana ujuzi wa miaka mingi kwenye maduka ya Supermarket, anachukua mahala pa Daniel Ndirangu, aliyeondoka mwisho wa mwaka jana. Okumu sasa anamulikwa kuona jinsi atakavyofufua maduka ya Tuskeys amabayo inakabiliwa na hatari ya kuporomoka.

 

KWALE; Ukulima kwa kiangazi umepigwa jeki na serikali.

Kwenye kaunti ya Kwale, Serikali ya Kaunti ya Kwale imeanza kukagua miradi ya maendeleo, inayolenga kuwainua wanawake kwenye masuala ya kilimo-Biashara.

Kulingana na Naibu gavana wa Kwale Fatuma Achani, uchimbaji wa mabwawa ni kati ya miradi inayotekelezwa na serikali ya kaunti, ili maji ya mabwawa haya yatumike kufanya kilimo.

Kama serikali ya kunti tunafanya kila tuwezalo kuwaona wanawake wanazingatiwa katika ukuaji wa uchumi wetu, tayari  kuna mabwa yamechimbwa tayari, maengina tunaendelea kuchimba ili wakulima wa Kwale wapate maji ya kufanyia kilimo hata nyakati za kiangazi” alieleza Bi Fatma.

Vile vile Bi Fatuma anelezea kuwa maafisa wa kaunti wanaendeleza mpango wa kutoa mafunzo ya ukulima kwa wanawake, wanaojihusisha na ukulima Kwale,kando na zoezi la ugavi wa mbegu za mahindi ili kuimarisha kilimo.