Kenya inatazama kufungua kituo cha kuuza Chai yake China.

Kenya imeweka nia ya kufungua kituo cha usambazaji wa chai yake  katika mkoa wa Wuyishan nchini China – ambapo baadhi ya chai ghali zaidi ulimwenguni hupandwa,kufuatia mahitaji ya chai ya Kenya katika uchumi wa Asia.

Thamani ya mauzo ya chai ya Kenya kwenda China ilipungua kwa zaidi ya theluthi moja mwaka jana licha ya kuongezeka kwa umaarufu wa chai ya maziwa ambayo imeongeza mahitaji ya majani ya chai nyeusi ama chai ya mkandaa kulingana na takwimu za biashara.

Shirika la Kuhamasisha uuzaji wa bidhaa za Kenya  nje ya nchi  (Keproba), linasema kuwa linapanga kufungua  “soko la chai ya  Kenya huko Wuyi” kama sehemu ya mikakati ya kusaidia wafanyabiashara wadogo na wa kati “kupata viwango vyao katika soko kubwa la Wachina”.

Kulingana na data inayohifadhiwa na Kituo cha Biashara cha Kimataifa (ITC). Kenya ilipata $ 3.17 milioni (KSh343.59 milioni) kutoka kwa uuzaji wa chai nyeusi i ulimwenguni mnamo 2019, asilimia 34.05 chini  ikilinganishwa na mwaka 2018

Takwimu hizo pia zinaonyesha kuwa Mwaka wa 2016  thamani ya chai ya Kenya ilifikia $ 1.77 milioni (KSh191.85 milioni), kabla ya kupanda hadi $ 2.5 milioni (Sh270.97 milioni) mnamo 2017 na $ 4.81 milioni (Sh521.35 milioni) mnamo 2018.

Ingawa China sio miongoni mwa maeneo 10 bora ya kununua  chai ya Kenya – inayoongozwa na Pakistan, Misri, Uingereza, Sudan na Urusi – lakini inaonekana kama soko linaloibuka na uwezo mkubwa wa kununua bidhaa hiyo kwa kiasi kikubwa zaidi ulimwenguni.