Hatimaye Seremala watabasamu nchini- Habari Mseto

Seremala nchini kupewa tenda na Serikali kuu.

Je, wewe ni Seremala?

Serikali kuu  linawaalika Seremala kote nchini  kujiandikisha na Makamishna wa Kaunti ili kuzingatiwa kwa  zabuni ya usambazaji wa madawati ya shule za umma kabla ya kufunguliwa.

Fundi hawa wanatarajiwa kuwasilisha maelezo ya mauzo yao ya kila mwezi ya mauzo, nambari zao za simu , maelezo yao  ya M-Pesa  na benki.

Warsha ya seremala chini ya sekta ya juakali  zitatambuliwa na kulipwa kupitia miundo ya msingi katika mfano sawa na ule uliowekwa katika Mpango wa Kazi Mtaani.

Mafundi waliochaguliwa watatoa madawati maalum iliyoundwa kusaidia wanafunzi kufuata itifaki za wizara ya afya almaarufu social distancing.

 

Pigo kwa Sekta ya Utalii

Idadi ya wageni kutoka nchi za kigeni nchini ilipungua kwa  asilimia 91.2 mwezi uliopita wa Agosti  ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana, kutokana na hofu ya maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19

Takwimu kutoka Taasisi ya Utafiti wa Utalii inaonyesha kwamba Kenya ilipokea watalii 14,049 mnamo Agosti – mwezi wa kwanza baada ya kufunguliwa kwa safari za ndege za kimataifa na za ndani ikilinganishwa na idadi ya watalii  159,804 wa kimataifa katika kipindi kama hicho mwaka jana.

Takwimu hizo pia zinaothibitisha kuwa kiasi cha watalii 6,368 au asilimia 45 hawakuja kwa kujinvinjari nchini ila  kutembelea marafiki na familia , ila 3,685 walikuwa likizo wakati tasnia ya utalii ilianza kurudi taratibu kwa shughuli mwezi uliopita.

Wengine 2,335 walikuwa wasafiri wa kibiashara wakati 1,129 walikuwa wakisafiri kwenda nchi zingine kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Moi hapa  Mombasa.

Kenya ilisitisha safari zote za ndege za kimataifa na za nyumbani mnamo Machi ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa coronavirus, hatua ambayo ilisababisha sekta ya utalii kupoteza Sh80 bilioni amabyo huchangia asilimia 10 ya pato la kitaifa.

 

Nchi kukopa zaidi.

Utawala wa Jubilee inatazamia  kukopa wastani wa Sh2.5 bilioni kila siku kabla ya kumalizika kwa muhula wa mwisho wa Rais Uhuru Kenyatta mnamo Agosti 2022.

Usimamizi katika  Hazina ya Bajeti ya kitaifa  inalenga kuchukua  mikopo mpya ya Sh1.87 trilioni katika miaka miwili hadi Juni 2022 au Sh2.5 bilioni kila siku, hatua ambayo itasukuma deni la nchi hadi hadi Sh8.06 trilioni.

Ikiwa hiyo itatimia,Rais  Kenyatta atakuwa amekopa angalau Sh6.1 trilioni kutekeleza miradi yake katika miaka 10 akiwa uongozini, alipochukua hatamu yake Juni  2013, Kenya ilikuwa na deni la Sh1.89 trilioni katika serikali ya pamoja kati ya Raila na Kibaki

Kutokana na deni hili kubwa,  Kenya inatoa  zaidi ya nusu ya ushuru iliyokusanyawa na KRA  kulipa mkopo, hali inayoacha pesa kidogo kwa ajili ya kujenga barabara, nyumba za bei rahisi na kuimarisha sekta ya afya.