Bima ya kuwanusuru waajiriwa waliopoteza ajira zao ghafla ibuniwe- KAM

Mkurugenzi mkuu wa KAM Phyllis Wakiaga

                                                 (Mkurugenzi mkuu wa KAM; Phyllis Wakiaga)

Chama cha Watengenezaji wa Bidhaa nchini almaarufu kama  Kenya Association of Manufacturers (KAM) wakiongozwa na mwenyekiti wao Dkt.Simon Githuku, imependekeza kuundwa kwa mfuko wa bima  kwa waajiriwa nchini  ili kuwanusuru  wafanyikazi watakaopoteza ajira zao kwa njia tatanishi zisizotarajiwa kama janga la COVID-19.

Katika pendekezo hilo, (KAM) kinasema mpango kama huo utahakikisha  kuwa wafanyikazi ambao watasistishwa ajira zao kazini ghafla  wakiendelea kujisetiri  kimaisha na familia zao wakitafuta ajira kwengine.

Muungano huo unadokeza kuwa mpango huo  wa bima unaweza kufadhiliwa kwa ushirikiano kati ya mfanyikazi na mwaajiri  sawa na michango kwa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii almaarufu National Social Security fund  (NSSF) ama hazina ya kitaifa.

Pendekezo hili  iliyoundwa na KAM  kwa ushirikiano na vyama vya kutetekea haki za wafanyakzi nchini, inatoka wakati takwimu kutoka Ofisi ya Takwimu ya Kitaifa ya Kenya (KNBS) zinaonyesha idadi ya watu walioajiriwa ilishuka hadi milioni 15.87 kati ya Aprili na mwisho wa Juni ikilinganishwa na milioni 17.59 kati ya Julai na Agosti.

Karibu wafanyikazi milioni 1.72 walipoteza kazi katika miezi mitatu kati ya Machi na Juni, Nchi ya Kenya ilipokuwa katika kilele ya kupambana na janga la virusi vya korona katika uchumi wake.

 

Waaajiri wanafaa kuanzisha mfuko wa bima  kwa waajiriwa ili kuwapiga jeki wafanyakazi watakao poteza kazi zao ghafla bila kutarajia, haifai mfanyakzi akipoteza kazi leo kesho ni ombaomba” Ilisoma sehemu ya ripoti hyo

Dakta Githuku  anapendekezea vyama  vingi vya wafanyakazi  kuja na maoni nyingi juu ya jinsi mpabgo huu unaweza kubuniwa na kufanikishwa nchini.

Ukifikia umri wa kustaafu , janga  kama sasa Corona au mzozo mwingine  kazini, tayari una kile cha kuanzia maisha kama sehemu ya pensheni yako.” Alieleza katika ripoti hiyo.

 

KAM inapendekeza kuzingatiwa mfumo wa Hazina  ya usalama  kwa wafanyakazi nchini Ujerumani inayofadhiliwa na serikali inayojulikana kama KURZARBEIT, ambayo huwahakikishia  mishahara waajiriwa  hata wakati wa majanga ya kuyumbisha uchumi wa nchi hiyo kama sasa.

Ufaransa, Italia, Ubelgiji, na Uholanzi ni miongoni mwa nchi zingine za Uropa ambazo zinaruhusu kampuni zenye shida kupata pesa za serikali kulipa mishahara katika vipindi vyenye mapato ndogo ama majanga ya kiuchumi.