"> Changamoto za COVID-19 kwa Uchumi wa taifa – Salaam Fm

Changamoto za COVID-19 kwa Uchumi wa taifa

Janga la Covid 19 linaonekana kutesa sekta kadhaa nchini, wengi  wakionekana kuachishwa kazi kutokana na hali mbovu ya uchumi, sekta ya utalii ikionekana kuguzwa zaidi.

Takwimu kutoka Ofisi ya Takwimu ya Kitaifa ya (KNBS) inaonyesha kuwa idadi ya Wakenya wasio na kazi umeongezeka hadi 4,637,164 kati ya Aprili na Juni, kutoka 2,944,724 katika kipindi cha Januari-Machi, kumaanisha kuwa kwa miezi mitatu pekee wakenya milioni 1.7 wamepoteza kazi zao.

Kutokana na hali hii, wanauchumi nchini  wanatoa wito kwa serikali kuweka mikakati itakayoinua uchumi wa taifa na kuziba mianya iliyopo kwa sasa. William Ramogi ni mshauri na mtaalamu wa uchumi nchini.

 Serikali inafaa kuanza kutafta njia ya kuimarisha uchumi wa nchi, kwa sasa walioajiriwa wengi wana zidi kupoteza kazi zao, uchumi nao ukidorora, bila mpango maalumu huenda tukapiga hatua nyingi nyuma kama taifa.”