"> Mgomo wa leo 2 Sept. umehairishwa kwa Muda- (KCGWU) Mombasa – Salaam Fm

Mgomo wa leo 2 Sept. umehairishwa kwa Muda- (KCGWU) Mombasa

Afueni kwa mkaazi wa Mombasa, Muungano wa wafanyakazi ukifutilia mbali makataa ya mgomo.

Muungano wa chama cha kutetea  maslahi ya wafanyakazi wa kaunti nchini (KCGWU) wakiongozwa na  Katibu mkuu nchini Bw. Roba Duba, umesitisha kwa muda agizo la  mgomo kwa wafanyakazi wa kaunti ya Mombasa iliyoratibiwa       kungo’a        nanga  hii      leo  2 Septemba, kushinikiza serikali ya Kaunti ya Mombasa kutimiza baadhi ya matakwa yao wanayohisi kupuuzwa kwa muda sasa kinyume na mktabata wao wa kazi.

Akiongea na wanahabari baada ya muktano  wa 28 Agosti uliochukua zaidi ya masaa manne ndani ya ukumbi katika ofisi za  bunge kaunti ya Mombasa,  Bw Duba  amekiri kwamba Serikali ya Kaunti ya Mombasa ikiongozwa na naibu Gavana  Dr. William K. Kingi na Katibu mkuu wa kaunti  Bw. Denis Lewa, imekubali  kwa sauti moja  kutimiza mapendekezo ya  muungano wa wafanyakazi  na kuwataka wanachama wao wote kutoshiriki maandamano au mgomo wa aina yoyote wanaposubiri   kutekelezwa kwa maazimio ya mkutano wao.

 Kwa sasa tumekubaliana hakuna mfanyakazi yeyote ataenda mgomo, hapa tuna washikadau wakuu wa kaunti, waweka hazina, Katibu mkuu na Naibu Gavana mwenyewe amekuwa kwa mkutano huo. Tumeafikiana kwa baadhi ya mambo na nina imani kuwa wafanyakazi wetu wametetewa ipasavyo” alieleza Bw. Duba.

Kauli yake ikiungwa mkomo na Katibu mkuu tawi la Mombasa Bw. Haji Mwinyi.

Kama katibu mkuu wa wafanyakazi tawi la Mombasa, tumehakikisha kwamba wafanyakazi wametendewa haki, tuliweka makataa ya mgomo ifikapo tarehe 2 Septemba, ila leo natangaza tena kuwa baada ya mkutano na washikadau katika serikali ya kaunti, tumesitisha kwa muda makataa hiyo, tunawaomba wafanyakzi wote wa Mombasa Kaunti kufika kwa vituo vyao vya kazi tukitarajia kuwa maazimio ya leo itatekelezwa”  alisema  Bw. Mwinyi.

Kwa ujumla, mkutano huo ambao ulitarajiwa kuamua hatima ya mkaazi wa Mombasa kuhusu maswala ya huduma kutoka kila sekta chini ya usimamizi wa kaunti kuanzia afya hadi mazingira, ulihudhuriwa na Naibu Gavana wa Mombasa, Katibu mkuu wa Kaunti ,Mwanakamati ya hazina ya kaunti, Afisa msimamizi katika ofisi ya Ugatuzi na utawala ya umma, Afisa mkuu wa fedha na Mkurugenzi mkuu wa huduma ya umma.

Kwa upande wa Muungano wa wafanyakazi ulihudhuriwa na  Katibu mkuu wa muungano wa wafanyakazi wa kaunti (KCGWU), Mwenyekiti  mkuu tawi la Mombasa, Katibu mkuu tawi la Mombasa, Naibu Mwenyekiti miongoni  mwa maafisa wengine walioteuliwa.

Kulingana na Bw. Roba Duba na mwenzake tawi la Mombasa Bw. Hajji Mwinyi, serikali ya kaunti ilikubali kutimiza maazimio yafuatayo;

  • Ya kwamba kwa muda wa wiki 2, serikali ya kaunti itakuwa imewasilisha kwa tume ya mshahara ya wafanyakazi (SRC) stakabadhi zote hitajika za wafanyakazi wake.
  • Serikali ya kaunti iandae mkutano kwa muda wa siku saba na washikadau wa chama cha kutetea maslahi ya wafanyakazi kujadili matokeo ya SRC
  • Yakwamba Usimamizi wa huduma ya umma wa kaunti kufuatilizia kwa ukaribu  stakabadhi zitakazo tumwa SRC ili kupata majibu upesi kutoka SRC
  • Mwafaka wa majadilaiano uwekwe wazi kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2021/2022 baada ya kuthibitisha CBA.

Kwa pamoja, Serikali ya kaunti pia ilikubali kulipa na kumaliza deni za wafanyakazi katika bima ya afya, kulipa mshahara kwa wakati, kumaliza malipo ya uanachama wa wafanyakazi kwa (KCGWU) wa  mwezi wa Juni na July,  miongoni mwa maazimio mengine yaliyowasilishwa na muungano wa wafanyakazi.