"> Fukwe za bahari Hindi Zaangamiza Maisha, Diani – Salaam Fm

Fukwe za bahari Hindi Zaangamiza Maisha, Diani

Mwanamume mwenye umri wa  miaka 26 amekufa maji baada ya kusombwa na mawimbi makali baharini  alasiri jana.

Kisa hichi kimefikisha jumla ya vijana sita waliokufa maji katika fukwe kuanzia mwezi Juni mwaka huu kufikia sasa

Mwendazake Bakari Hamisi Baluna mkaazi wa kijiji cha Malalani Ukunda alikuwa ameandamana na nduguye baharini katika eneo la Trade winds kabla ya kuzidiwa na maji na kusombwa na mawimbi ya bahari .

Aidha watano walio salia walikuwa wanafunzi ambao hufanya mazoezi katika fukwe hizo za bahari na baadaye kuogelea

Shughuli za kuokoa mwili wake zimechukua zaidi ya masaa 16 kutokana na kuchafuka kwa bahari ambazo ziliendeshwa na kikosi maalum cha wapigambizi Diani Maarufu kama Diani Water Guard na kufaulu kuupata mwili huo katika bahari kuu.

Kulingana na Clara Mulwa mpiga mbizi katika kikosi hicho amewataka wenyeji wanaotumia fukwe za bahari ya kwale kuwa makini katika kipindi hichi ambacho bahari imechafuka kwa mawimbi makali.

Hata hivyo mipango ya kupiga marufuku watu kuogelea katika bahari ya hindi eneo hilo la trade winds imeanza kutokana na mchafuko wa bahari kunzia mwezi uliopita na kuwepo kwa mawimbi makali.