"> Wafanyakazi wa hoteli za kitalii watasubiri zaidi ufadhili kutoka kwa serikali. – Salaam Fm

Wafanyakazi wa hoteli za kitalii watasubiri zaidi ufadhili kutoka kwa serikali.

                                                                                                   The Boma Nairobi Tourist Hotel 

Wizara ya utalii ingali haijatoa shilingi bilioni 2 za kuwasaidia wafanyakazi wa hoteli  walioathirika  na makali ya korona baada ya mahoteli kufungwa.

Katibu katika wizara ya utalii Safina Kwekwe amesema kwamba wizara hiyo imepokea shilingi Bilioni 3 za kuwawezesha wamiliki wa mahoteli kuboresha sehemu za kitalii ila si za kuwafadhili wafanyakazi wa hoteli.

Hata hivyo Katibu Kwekwe amesema tayari mikakati ya kufuatiliaa fedha hizo inanendelea ili kuhakikisha kwamba wafanyakazi hao wanasaidika huku wakisuburi kuimarishwa kwa sekta ya utalii nchini.

Pesa ambayo wizara ilitengea hoteli ya bilioni 3 ni za kukarabati na kurejesha hali nzuri ya hoteli na sehemu za utalii zetu, kwa sasa tunatathmini namna ya kuwasetiri wafanyakazi wa hoteli hizo ila bado pesa haijatoka, tunaomba uvumilivu kwenu” Bi. Kwekwe alisema.

Kauli ya katibu huyo inawadia baada ya chama cha kutetea maslahi ya wafanyakazi wa hoteli nchini, kudai kucheleweshwa kwa fedha hizo za kuwasetiri wafanyakazi wa hoteli nchini.

 Mzungu hawezi taka kuja Kenya kukaa kwa jengo lililopakwa rangi na hakuna mfanyakazi, lazima maslahi ya wafanyakazi wa hoteli iwekwe kipaumbele ndio tuanze kukarabti hoteli zenyewe, tunaumia kwa sasa, hatuna kazi na tuna familia ambao wanataka chakula