Pigo kwa masoko ya chai India, ya Kenya yakinawiri.

Viwango vya chini vya bei  ya chai katika soko la mnada mjini Mombasa inaendelea kuwavutia  wanunuzi wakuu kote ulimwenguni huku wafanyabiashara katika soko hilo wakithibitisha kuendelea kuvuna pakubwa licha ya changamoto za ugonjwa wa COVID-19.

Kwa mfano, nchi  za Pakistan, Uingereza, Misri na nchi za Mashariki ya Kati wameanza kuagiza chai zote kutoka soko la mnada la Mombasa bila kuagaiza vifurushi vingine kutoka  India ambayo imekuwa ikipa Kenya Ushindani mkubwa katika soko la Majani chai.

Takwimu kutoka kwa ofisi ya Mkurugenzi ya soko la mnada la Mombasa zinaonyesha kuwa idadi ya mauzo yao  imekuwa ikipanda tangu Aprili ikilinganishwa na kipindi sawa mwaka jana.

Pakistan iliongeza agizo lake  kwa asilimia 14 mnamo Mei na asilimia 18 mnamo Juni wakati Uingereza ikiongezeka hadi asilimia 66 Mei na asilimia 12 mwezi Juni.

India ni mzalishaji wa pili mkubwa wa chai ulimwenguni  nyuma ya China, Kenya ikishikilia nafasi ya nne nyuma ya Indonesia kote ulimwenguni.

Kwa sasa, kutokana na kupungua kwa soko la la Majani chai nchini India , kuna hofu kuwa huenda ikapoteza takriban asilimia 16 ya pato lake katika soko la majani chai kwenye  historia yake tangu kufungua milango ya soko la nje.