Wabadhirifu wa fedha za Corona kikaangoni

Tume ya maadili na kukabili ufisadi EACC imesema itawawajibisha maafisa wote wanaokabiliwa na tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za kukabili janga la virusi vya korona kwa mujibu wa sheria.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Tume hiyo imesema kwamba tayari wafanyakazi 3 waliokuwa wakihudumu katika bodi ya mamlaka ya kusambaza dawa nchini KEMSA wameachishwa kazi kwa muda ili kupisha uchunguzi dhidi ya matumizi mabaya ya fedha za ununuzi wa maski pamoja na vifaa vyengine vya kujikinga na maambukizi.

Hata hivyo EACC imeongeza kwamba inaendelea kuchunguza madai ya matumizi mabaya ya fedha katika Mamlaka ya usambazaji dawa KEMSA.