Wafanyabiashara katika soko la Mackinon kaunti ya Mombasa wameelezea jinsi bidhaa za ndimu na limau zimepanda bei maradufu na hata kukosekana katika masoko mbali mbali nchini kufuatia kuzuka kwa janga la virusi vya Corona.

Kulingana na wafanyabiashara katika soko hilo, imekuwa vigumu kupata bidhaa hizo licha ya kupanda bei kwa bidhaa hiyo.

Wafanyabiashara hao aidha wameongeza kuwa licha ya kuwa ndimu zinapatikana katika ukanda wa Pwani kukosekana kwa bidhaa hiyo kumesababisha kuagiza nchi jirani.