Sitisheni safari za kuenda Kenya, Marekani imeonya raia wake.

Nchi ya Marekani imewaonya raia wake dhidi ya kusafiri Kenya kutokana na hatari ya COVID-19

Marekani iliwatahadharisha raia wake dhidi ya kusafiri nchini Kenya kutokana na hali ya kiafya.

Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Marekani (CDC) kilitambua kuwa serikali ya Kenya imelegeza masharti ya kuzuia maambukizi ya COVID-19 na hivyo huenda raia wake wakawa kwenye hatari wanapokuwa nchini humu.

Hata hivyo, ingawa nchi ya Marekani inawaonya raia wake  dhidi ya kusafiri nchini Kenya kwa kuwa ni hatari kutokana na virusi vya Corona, kinaya ni kuwa, visa vya corona nchini Marekani vimezidi milioni tano kufikia Jumamosi, Agosti 8, na zaidi ya vifo 160,000 na kuiweka miongoni mwa nchi zilizoathirika zaidi ulimwenguni kutokana na virusi hivyo.

CDC pia ilisema itakuwa vigumu kwa raia wake kupata matibabu bora endapo wataambukizwa  kutokana na uhaba wa vifaa vya kutibu homa ya corona Kenya  ilivyoripotiwa na waziri wa afya  Mutahi Kagwe.

Kwa sasa,Marekani kupitia (CDC) imewashauri raia wake kuzingatia  tahadhari kwa  kujiepusha na usafiri wowote ambao sio wa dharura kuenda Kenya hasa raia wake wenye changamoto za kiafya.

Stisha kusafiri Kenya kwa sababu ya COVID-19. Wasafari wamo kwenye hatari kubwa ya kuugua zaidi kutokana na COVID-19 . Nibora kusitisha kwa muda usafiri wowote isiyokuwa wa dharura  kuenda Kenya,” ilionya CDC.

Mapema mwezi huu,nchi ya Kenya iliorodhesha mataifa ambayo ndege zake zitaruhusiwa kusafiria  kutokana na janga la COVID-19. Katika orodha hiyo, ndege kutoka Marekani, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Netherlands, Qatar, Muungano wa Mataifa ya Uarabuni na Italia ambayo yalikuwa yamepigwa marufuku kuingia Kenya yaliruhusiwa kurejelea safari zake nchini humo.

Kufikia sasa  Idadi ya visa vya COVID-19  nchini  yamepita 26,000, vifo 420 na waliopona kuwa 12,961.