Kutana na Jeniffer Muema, mfano wa tabasamu kwa ushindi wa Saratani.

Tarehe 11  Agosti  2014, itabaki katika kumbukumbuku za Mwalimu Jeniffer Muema, akuwe akisimulia kizazi chake na wanaohusika aushini mwake.

Kama mgonjwa yeyote anayemtembelea daktari  kutafuta ushauri wa hali ya afya,  kwa Jeniffer , ilikuwa mwamko mpya, siku ya kuanza hatua mapya katika mkondo tofauti wa maisha ambayo bila kubisha, mhusika hana hiari kutii.

Anasimulia kwa huzuni ilivyokuwa siku yenyewe,  namna matokeo ya daktari yalivyoonyesha anaugua saratani ya kizazi yaani  cervical cancer kisha baadaye saratani ya mfuko wa uzazi almaarufu Uterine cancer.

Daktari aliponieleza matokeo ya hali yangu, mwanzo sikuamini, nilitaka arudie utaratibu wa kupima tena na tena, nilidhani nimefika mwisho wa maisha yangu, hata sikujua hali yangu itapokelewa vipi kwa familia yangu, hasa watoto wangu ” Alieleza Jeniffer.

Ilivyotarajiwa ,Jeniffer aliachwa kwa mtanziko, asijue amwelezee nani hali yake na akamwache nani, hakuweza tabiri atakavyopokelewa  kwa familia yake, marafiki na hata majirani.

Picha za washirika wa Wakfu ya Jeniffer Cancer Foundation

Kwa kutambua kuwa hana tena njia mbadala, Jeniffer anaeleza alivyopiga moyo konde na kuukubali yaliyompata; yajapo yapokee. Akawaelezea familia, marafiki na hata walimu wenzake, wote kwa pamoja wakamkubali na kuukumbatia hali yake mpya.

Kinyume na familia zingine za waathiriwa wa saratani, familia yake ilipokea habari za ugonjwa wake kwa huruma na  kuanza kumsaidia katika kila hatua ya safari ya kurejesha maisha yake ya awali.

Pesa za usafiri kuenda na kurudi kwa daktari wake ambaye alikuwa  Nairobi,  ilikuwa miongoni mwa changamoto ambazo alikuwa anapitia, huku akiishi kwa mafikira ya namna ya kupata uwezo wa kumudu gharama ya dawa na mahitaji mengine.

     “Mwanzoni hali haikuwa wa kustahimilika, usiku na mchana zangu zilikuwa dhiki”

Kulingana na maagizo ya daktari, Jeniffer alitakiwa  kusafiri jijini Nairobi mara tatu kwa wiki, sikuambii maumivu na unyanyapaa wa wanaoshikilia kuwa saratani ni breki ya mwisho wa maisha.

Anasimulia kwa masikitiko ugumu aliyoupitia siku zake za mwanzo alipoanza  kuugua saratani hadi alipoanza kuona ahueni na kuzoea hali hata ingawa vibayavibaya.

Kwa sasa miaka sita yamepita tangu kuanza kukabiliana na nduli huyu saratani, ila leo Jeniffer anasimulia tabasamu lake limerejea, hali yake imejirudi, hana tena majonzi, safari zake za kila mara kwa daktari kwa kila kona ya Kenya zimepungua pengine akihisi mabadiliko tu mwilini kulingana na malezo ya daktari.

Ni kutokana na ugumu na hali ya dhiki aliyoyapitia Jeniffer alipoanza kutafuta nusura ya saratani ndipo alipoanza kutafakari namna anvyoweza rudisha tabasamu kwa waathirika wa gonjwa hili katili ambalo kulingana na takwimu za shirika la afya ulimwenguni WHO, hufisha zaidi ya watu milioni 30,000 kila mwaka nchini Kenya na zaidi ya watu milioni 9.4 kote ulimwenguni kila mwaka.

Kulingana na Jeniffer Mwema ,uzinduzi wa wakfu wa  Jeniffer Cancer Foundation , ulikuja kama mmoja wapo wa njia ya kuwahamasisha na kuwapa uasaidizi tahijika wagonjwa wa saratani ambao Jeniffer anahisi hawafai tena kupitia changamoto na madhila aliyoyapita yeye alipokuwa katika kilele cha kuugua saratani.

Ashley Mutava, Nelly Medza (waliojitolea) na Betty Mumo( picha ya ndani) Mfadhiliwa                                               

Tangu kufungua milango ya wakfu yake hii  ambayo ina makao makuu mjini Mombasa na matawi mengine  kote nchini Kenya,  Jeniffer anaeleza kuwa  kwa uwezo wao finyu wa kifedha, malazi na chakula, wameweza kuwashika mikono zaidi ya wagonjwa 2,000 ila kwa sasa dhoruba ya COVID -19  imelemaza juhudi zao kwa pakubwa.

Kama wakfu, tulikuwa tukiwatembelea wenzetu popote walipo, ingawa kwa sasa tumefilisika, hatuna tena uwezo kuendeleza mipango yetu, nina huzuni kumwona mwathiriwa anahangaika. COVID-19 imefanya hatuwezi kutembeleana wala kutisha mikutano tena” Alikiri Jeniffer.

Kwa niaba ya wakfu ya Jeniffer Cancer foundation, anaomba msaada wa pesa ama mahitaji mengine  kwa wategemezi wao ambao licha ya ugumu wa maisha,wanaishi kutegemea wakfu hii kwa kila aina ya usaidizi, ikiwemo dawa za kupunguza makali ya maumivu.

Kusema ukweli unavyoniona sasa, hatuna hata peni kwa akaunti yetu, hatuna hata cha kununua paracetamol, tunaomba msaada, yeyote tunamwalika kutusaidia, hata kugharamia usafiri wa njia moja kumpeleka mgonjwa kwa daktari Nairobi ama Eldoret, .Baadhi ya wategemezi wetu sasa wamedhoofika kiafya kwa kukosa gharama ya matibabu, wengine tumewazika” Alisema kwa huzuni

Picha ya mahasibu wa saratani kutoka Jeniffer Cancer Foundation

Mawasiliano ya Wakfu ya Jeniffer Cancer foundation ni;

Changamwe-msikiti noor, Mombasa

www.jeniffercancerfoundation.org

info@jeniffercancerfoundation.org

+254 723 343 464

Ili kupiga jeki juhudi za J.C.F, tumia ;

Bank Account Details;

A/C: JENIFFER CANCER FOUNDATION

Account no.1266257365

KCB BANK
TREASURY BRANCH

               Ama kupitia Paybill no: 205270