KEMRI na matabibu wa Kienyeji waungana

Mtafiti wa shirika la utafiti la KEMRI Marry Bitta amesema kuwa asilimia kubwa ya watu walio na matatizo ya akili hawaendi hospitali  kutafuta matibabu katika kaunti ya Kilifi bali hutafuta matibabu kutoka kwa madaktari wa kienyeji.

Bitta amesema kuwa kulingana na takwimu za shirika la afya duniani WHO mmoja kati ya watu wanne siku moja katika maisha yake atapatwa na matatizo ya akili.

Aidha amongeza kuwa shirika hilo kwa sasa limeungana na matabibu wa kienyeji ili kuhakikisha wanafaulu kutibu ugonjwa wa akili.