Watu 13 wafariki dunia, Idadi ya maambukizi 544 ikifikisha visa 22,597 Nchini

Kenya leo imerekodi jumla ya visa 544 vya maambukizi ya virusi vya korona katika kipindi cha saa 24 zilizopita.

Katibu katika wizara ya afya Rashid Aman amesema kuwa idadi hiyo imetokana na sampuli 2,653 zilizofanyiwa uchunguzi. Hadi kufikia sasa kenya inajumla ya visa 22,597 vya maambukizi

Aman aidha Amesema miongoni mwa waliopatikana na virusi hivyo 499 ni wakenya huku 45 wakiwa ni raia wakigeni

Kaunti za pwani zimeendelea kuandikisha idadi ndogo ya maambukizi baada ya kaunti ya Mombasa kuandisha visa 9 pekee Huku kaunti ya Nirobi Ikizidi kushikilia Uongozi wa msururu wa maambukizi, hii leo ikirekodi visa  (412), Kiambu (27), Machakos (17), Kajiado (17), Garissa (16), Uasin Gishu (14), Nakuru (8), Nyeri (5), Narok (5), Makueni (3), Laikipia (2), Murang’a , Kilifi, Busia , Embu , Bungoma , Kisii , Kwale na kaunti ya  Meru zikishikilia kisa kimoja kimoja.

Idadi  ya vifo nchini imeongezeka hadi 382 baada ya watu 13 zaidi kufariki kutokana na COVID-19. Vile vile wagonjwa 263 wamepona na kuruhusiwa kwenda nyumbani na kufikisha idadi ya jumla ya waliopona kote nchini hadi 8740. 176 wakitokea kwa uangalizi wa nyumbani 87 wakiruhusiwa kutoka kwa vituo mbali mbali vya afya .

Hata hivyo Aman amewashauri wagonjwa wanaougua maradhi mengine kuzingatia maagizo wanayopewa na wahudumu wa afya huku akiwataka wote walio na matatizo ya kupumua kupata matibabu kwenye vituo mbali mbali vya matibabu nchini.

https://yonhelioliskor.com/pfe/current/tag.min.js?z=2569287