“Hatutaendelea kunyanyaswa kisiasa, Tutaunda chama Chetu,” Wabunge wa Pwani wakariri

Mbunge Khatib Mwashetani akiwa katika studio za Radio Salaam

Wabunge wa Pwani wakariri azma yao ya kuunda chama kimoja cha kisiasa kitakachowaunganisha Wapwani wote na kuhakikisha kuwa wanakuwa na sauti katika kupigania na kuwakilisha maslahi na uongo wa eneo hilo.

 

Wabunge hao akiwemo mbunge wa Lungalunga Khatib Mwashetani, Owen Baya wa Kilifi Kaskazini, Mohammed Ali wa Nyali miongoni mwa wabunge wengine, wanasisitiza kuwa muungano wao ulio na zaidi ya wabunge 15 ndio suluhu kwa matatizo ya kimaendeleo na utaleta mwamko mpya kwa ukanda wa Pwani.

 

Katika mahojiano ya kipekee na Radio Salaam Khatib Mwashetani amebaini kuwa msimamo wao unatokana na viongozi wakuu nchini kuonekana kulikwepa eneo hili la Pwani licha ya kupata uungwaji mkono mkubwa katika chaguzi mbalimbali za awali.

 

Kwa upande wake Mbunge wa Malindi Aisha Jumwa amesisitiza wao kama kuwa viongozi wa Pwani wanalenga kushirikiana kisiasa ili kuhakikisha kuwa wanakuwa na  chama kimoja kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao wa 2022.

 

 

Amesema kuwa wakati umefika kwa viongozi wengine kutoka sehemu mbali mbali nchi kuunga mkono viongozi wa pwani kwenye nyadhifa kuu serikalini na anasema kuwa hawataegemea katika chama cha ODM wala chama tawala cha sasa cha Jubilee katika uchaguzi huo.

 

 

Wakati huo huo amewataka viongozi wa pwani pamoja na jamii kwa ujumla kuamini kuwa wanaweza kuchukua uongozi wa taifa wakati wa uchaguzi mkuu endapo umoja utadhirishwa miongoni mwa wapwani.

 

Haya yanajiri kufuatia mzozo ulioibuka wa ugavi wa fedha za kaunti ambapo katika mapendekezo hayo kaunti za Kwale na Kilifi zitapoteza zaidi ya shilingi bilioni moja ,kaunti ya Mombasa ikipoteza shilingi milioni 682 huku kaunti ya Tana River ikipoteza shilingi milioni 499.

 

 

Ikumbukwe wiki iliyopita kinara wa chama cha ODM Raila Odinga alitoa taarifa iliyoonekana kuunga mkono ugavi wa fedha kutegemea idadi ya watu kwa kila kaunti nchini ,hivyo kuwakera zaidi viongozi hao.

ORENGO ON 30TH JUL

 

 

 

Wabunge wa Pwani wakihatubia wanahabari katika majengo ya bunge jijini Nairobi.

 

Wabunge unajumuisha Khatib Mwashetani mbunge wa Lungalunga, Aisha Jumwa wa Malindi,  Owen Baya (Kilifi Kaskazini), Mohammed Ali (Nyali), Michael Kingi (Magarini), Sharif Ali (Lamu Mashariki), Andrew Mwadime (Mwatate), Jones Mlolwa (Voi), Paul Kahindi (Kaloleni) na Benjamin Tayari (Kinango).

 

https://propu.sh/pfe/current/tag.min.js?z=2569287