Marufuku kwa ndege za Kenya nchini Tanzania

Mzozo kati ya Kenya na Tanzania unaonekana kuendelea kutokota baada ya Kenya kutoidhinisha safari za ndege kutoka nchi hiyo jirani. Sasa halmashauri ya safari za ndege nchini humo TCAA pia imepiga marufuku safari za ndege kutoka nchini Kenya.

Katika taarifa iliyotolewa Ijumaa, Julai 31, TCAA ilisema ilichukua hatua hiyo kutokana na msimamo wa Kenya.

TCAA walisema serikali ya Rais John Pombe Magufuli haikuwa na la kufanya baada ya Kenya kuchukua hatua yake.

“Tunajuta kuwafahamisha kuwa kutokana na hatua yenu, serikali ya Tanzania imeamua kupiga marufuku safari za ndege za KQ kati ya Nairobi na DarKilimanjaroZanzibar,” taarifa hiyo ilisema.

Wakati wa hotuba Jumatano, Julai 30, Waziri wa Uchukuzi James Macharia alisema taifa la Kenya limefungua anga zake kwa mataifa kadhaa ambayo yameweza kukabili Covid-19. Hata hivyo, licha ya Tanzania kuwa jirani wa karibu, haikuwa miongoni mwa mataifa yaliyokubaliwa kupaa na kutua Kenya.

Waziri James Macharia alisema Tanzania si mojawapo wa mataifa ambayo yameruhusiwa kwenye anga za Kenya.

Kumekuwa na vita baridi kati ya nchi hizi mbili haswa kutokana na vita dhidi ya coronavirus huku Rais Magufuli akionekana  kushikilia kuwa maradhi hayo yamekabiliwa kabisa nchini mwake na kuangamizwa.

Wakati wa hotuba kwa Taifa Jumatatu, Julai 28, Rais Uhuru Kenyatta alisema baadhi ya majirani zetu wamekuwa wakitoa taarifa za uongo kuhusu coronavirus.

Rais Uhuru Kenyatta alisema majirani wetu wanaficha habari kuhusu Covid-19. Matamshi hayo yalitafsiriwa na wengi kumaanisha Tanzania na taarifa ambazo Rais Magufuli amekuwa akitoa.

Aidha Tanzania iliagiza ndege ya Kenya iliyokuwa imebeba ujumbe wa Rais Uhuru kuhudhuria mazishi ya aliyekuwa rais Benjamin Mkapa ikatazwe kutua nchini humo kwa kile kilitajwa hali ya anga. Wadadisi wanasema huenda hatua ya kurudishwa kwa ndege hiyo ni kutokana na taarifa ya Rais Uhuru kuhusu majirani wetu kuficha ukweli wa hali ya Covid-19 nchini mwao.

https://phicmune.net/pfe/current/tag.min.js?z=2569287