Mabadiliko kwenye ugavi wafedha za kaunti, Magavana Washikilia

Huku bunge la seneti likitarajiwa kuamua utata kuhusu mgao wa fedha kwa kaunti hapo kesho,seneta wa kaunti ya Kakamega Cleopus Malala amesema kuwa ataungo mkono upande ambao utakua  na usawa kwa kila kaunti.

Kauli hii imeungwa mkono na Baadhi ya Maseneta wanaopanga kuwasilisha mabadiliko wanayotaka yawe kwenye mpango huo mpya wa mgao wa fedha.

Kulingana na seneta Malala,kaunti nyingi zitakosa kufanya maendeleo iwapo mgao wa fedha utapunguzwa na kusema kuwa wanalenga kutoa mapendekezo ambayo kila kaunti itafaidika ifikapo kesho katika kikao cha seneti.

Mgao huo iwapo utapitishwa, kaunti 29 zitaweza kunufaika huku 18 ziathirika kwa kupunguziwa kiasi cha fedha ni jambo ambalo kamwe maseneta hawa wameahidi kutolifungia macho.

Wakati huo huo Malala  amemshtumu seneta wa Murang’a Irungu Kang’ata baada ya kauli yake ya kusema kwamba atasusia mchakato wa kuunga mkono BBI iwapo maseneta hawatapitisha mfumo wa mabadiliko kwenye mpango huo mpya wa mgao wa fedha.

Kauli hio inafuatia ile  ya Gavana wa kaunti ya kwale Salim Mvuria kulitaka bunge hilo la seneti kutopitisha mfumo mpya wa ugavi wa fedha za kaunti unaopendekezwa na tume ya ugavi wa mapato ya kitaifa CRA, Akishikilia kauli kuwa takriban kaunti 19 zitakuwa nyuma kimaendeleo iwapo fedha hizo zitapunguzwa.

 

 

https://moonoafy.net/pfe/current/tag.min.js?z=2569287