Wahudumu Wa Afya katika kaunti ya Lamu kumtaka Gavana Twaha Kuwajibika

 

Gavana wa kaunti ya Lamu Fahim Twaha, amehimizwa kuangazia maslahi ya wahudumu wa Afya katika hospitali ya umma ya King Fahad.

Kulingana na Daktari mkuu wa hospitali hiyo Ali Abdallah, hali inayoikumba hospitali hiyo kwa sasa ni ya kusikitisha, kwa asilimia kubwa  wahudumu wa afya pamoja na wagonjwa wanaozuru hospitali hiyo kwa ajili ya  matibabu hujawa hofu ya maambukizi ya virusi vya Corona kutokana na hali ya wahudumu hao kukosa vifaa vya kujikinga.

Daktari Abdallah amemtaka gavana huyo kutafuta suluhu kwa haraka kwani huduma za matibabu katika hospitali hiyo zimelemaa na iwapo swala hilo litaangaziwa basi shughuli za matibabu zitarejea katika hali ya kawaida.